Mkuu wa Mkoa wa Kigoma CGF (Mst.) Thobias Andengenye amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikionesha Watu ambao wanatajwa kuwa ni Wafanyakazi wa ajira mpya za Serikali wakiwa wamechafuka baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza kazi katika vituo walivyopangiwa.
Andengenye amesema “Najua inaweza kuwa ni utani nimeona clip mbalimbali na picha zinatembea mitandaoni Watu wakiwa wamechafuka kwa vumbi na wameandika kuwa wameripoti vituo vya kazi Kigoma, tuzipuuze huu ni uzandiki sisi tumepita kwenye hizo barabara wanazozisema na tunafahamu vizuri mendeleo yetu, na tunaendelea kumshukuru Rais wetu Wakandarasi wanaendelea kuchapa kazi bila kusimama"
"Kigoma ya sasa sio kama ya zamani, hakuna Mkoa mwingine kuna kilometa zaidi ya 400 zinajegwa kwa kiwango cha lami zaidi ya Kigoma, pia kuhusu kuungana na Tabora tumebakiza KM 14 tu”
RC Andengenye amewahakikishia pia Watumishi waliopangiwa Kigoma kuwa ni sehemu salama na mazingira yake ni mazuri na rafiki kwa kila Mtu na wasipotoshwe na mitandao”