Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC ajitangaza kuambukizwa corona

Dkt RC ajitangaza kuambukizwa corona

Fri, 1 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, amejitangaza kuwa amepata maambukizo ya virusi vya corona baada ya kuamua kupima afya yake kwa hiari bila ya kuwa na dalili zozote.

Dk. Mghwira alithibitisha hilo juzi, akibainisha kuwa baada ya mizunguko mingi ya kufuatilia mwenendo na hali ya maambukizo ya corona mkoani mwake na kukutana na makundi mengi ya wananchi, aliamua kupima afya yake.

“Niliona ni vizuri kupima ili kuangalia afya yangu, niliamua kufanya hivyo kwa sababu kazi yangu inaingiliana na watu.

“Nimepima na matokeo yameonyesha nimeambukizwa virusi vya corona. Sina dalili za corona, sina homa, wala sina chochote isipokuwa vipimo vimeonyesha hivyo," alisema.

Kiongozi huyo wa mkoa alisema watu wengi wanaweza wakawa wanatembea huku wakijiona wapo salama kumbe wana maambukizo, hivyo akawataka wapime kwa hiari kwa sababu ni muhimu.

Aliwaomba wananchi wa mkoa huo wazingatie masharti yanayotolewa na wataalamu wa afya kujinga na maambukizo ya virusi hivyo.

“Sokoni bado watu hawajazingatia uvaaji wa barakoa, watu wanakaa karibu, nilipokuwa nikienda kwenye makundi ya watu, nilikuwa naona kuna kitu kinaniingia, kikawa kinanipa hisia kuna tatizo,” alisema.

Dk. Mghwira alisema uzoefu wake mfupi wa kuishi na maambukizo hayo, umempa somo kuona kuna tija kwa wagonjwa kutunzwa nyumbani kuliko kwenye vituo.

“Ninasema hivi kwa sababu, kama mwanafamilia mmoja ameambukizwa nje au ndani, uwezekano wa kuambukiza wanafamilia ni mkubwa.

“Tukianza kutunzana nyumbani, itapunguza gharama na kusaidia kuimarishana kama familia kuliko mmoja akitengwa, ni kitu kigumu sana.

“Nimejaribu hapa katikati kuwaonyesha watu wote waliokuja karibu na mimi kwamba nimepima. Je, ikija nina maambukizo, unaonaje haiwezekani tu, huwezi ukawa umeambukizwa halafu uwe hivi, sasa niweje? Tunahitaji kujifunza kupokea mambo magumu," alishauri.

Dk. Mghwira ni kiongozi wa kwanza kujitangaza kupata maambukizo ya virusi hivyo nchini tangu serikali iliporipoti mgonjwa wa kwanza Machi 16 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live