Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aitaka NFRA kutafuta soko la mahindi

583d8f79715b99faf449c8b4a96f2d62 RC aitaka NFRA kutafuta soko la mahindi

Fri, 8 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo ameushauri Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula nchi ni (NFRA) kutafuta masoko ya uhakika yenye ushindani katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ili wakulima kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wanaozalisha nafaka kwa wingi hususani mahindi wafaidike na soko hilo.

Mikoa hiyo ni pamoja na Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa na Ruvuma.

Aidha licha ya wakala huo kuwa na mpango wa kuweka mfumo wa kisasa wa kuhifadhi nafaka kufikia asilimia 80,Wangabo aliishauri kujiandaa kununua mahindi mengi zaidi ili kuwahakikishia wakulima wa mikoa hiyo soko la mazao yao katika msimu wa ununuzi wa mahindi 2020/ 2021.

Alitoa ushauri huo hivi karibuni alipotembelea ujenzi wa vihenge vya kisasa vinavyoendelea kujengwa katika kijiji cha Kanondo katika manispaa ya Sumbawanga.

“Wakati umefika sasa NFRA wakaongeza fedha za kununua mahindi na kisha kutafuta soko nje ya nchi hasa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na nchi nyingine ili kuwapa fursa wakulima nchini kufanya biashara na NFRA ili kuepuka kuhangaika kutafuta soko la mazao yao,” alishauri.

Aliongeza kusema kuwa: “Mkoa wa Rukwa tumezalisha tani za mahindi 585,000 wakati mahitaji halisi ya ndani ni tani 291,000 hivyo tuna ziada ya tani 294,000 lakini NFRA Kanda ya Sumbawanga imenunua tani 11,000… mahindi mengi yalibaki mikononi mwa wakulima. Nategemea kwamba ukamilishwaji wa vihenge hivi NFRA itakuwa na uwezo wa kuchukua tani 58,500, hii kwa sisi mkoa wa Rukwa ni sawa na kuingiza na kutoa ili wawauzie watu wengine.”

Mhandisi Mkazi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Haruna Kalunga alisema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 80 .

Chanzo: habarileo.co.tz