Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aingilia kati mgomo wa daladala, bajaji Songwe

Bajaji Songwe (600 X 355) RC aingilia kati mgomo wa daladala, bajaji Songwe

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Dk Francis Michael ameagiza viongozi wa wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Kenani Kihongos kukaa na madereva bajaji pamoja viongozi wa dalala kutatua migogoro yao ya kusafirisha abiria katika mji wa Tunduma.

Mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo baada ya kukutana na madereva bajaji katika mji wa Tunduma waliokuwa wameandamana wakidai kuwa wamezuiwa kusafirisha abiria kutoka stendi ya Kilimanjaro kwenda mji wa Mpemba ulio nje kidogo pasipo wao kushirikishwa.

" Kwa kuwa mnasema mmesimamishwa pasipo kukaa kikao cha pamoja na viongozi, wa wilaya, Latra, Tanroad na kupitia kikao hiki natoa maelekezo kuwa endeleeni na utaratibu wa awali wa kusafirisha abiria kutoka Kilimanjaro mpaka mji mdogo wa Mpemba wakati tunasubiri kikao cha pamoja ," amesema. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live