Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aagiza watumishi 34 wakamatwe

BRIG RC aagiza watumishi 34 wakamatwe

Wed, 24 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, ameagiza kukamatwa kwa watumishi 34 wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, wakiwamo watendaji wa vijiji na kata kwa kushindwa kurejesha Sh. milioni 307 zilizokusanywa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani bila kupelekwa benki.

Alitoa hilo jana kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kagera, alipozuru wilayani humo kutoa maelekezo ya kiutendaji kutokana na halmashauri hiyo kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato, huku kukibainika ubadhirifu wa fedha za serikali.

Aliagiza kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi watumishi hao, mamlaka kuwasimamisha kazi Kaimu Mwekahazina, Sospiter Makene, maofisa wa TEHAMA, Jastine Banula na Rogers Semukoko pamoja na Ofisa Biashara, Beatrice Gurusya, wote watumishi wa halmashauri hiyo.

Gaguti amechukua uamuzi huo baada ya kutoa siku saba kwa watumishi hao kurejesha fedha hizo alipozungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika Juni 5 mwaka huu kwa lengo la kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Nilikuja hapa nikatoa maelekezo kwa wale wote waliokuwa wanakusanya fedha kwa kutumia mashine za Poss bila kuzipeleka benki kuwa warejeshe fedha na nikawapa siku saba, lakini fedha iliyorejeshwa ni asilimia mbili.

“Nilikuja hapa nikatoa maelekezo kwa wale wote waliokuwa wanakusanya fedha kwa kutumia mashine za Poss bila kuzipeleka benki kuwa warejeshe fedha na nikawapa siku saba, lakini fedha iliyorejeshwa ni asilimia mbili.

"Kwa mwendo huu, hatuwezi kwenda, lazima tuweke misingi imara ya kuboresha utumishi na uadilifu, hapa nina orodha ya watendaji 30 ambayo nampati Kamanda wa Polisi kuhakikisha watu hao wanakamatwa popote walipo na wengine wanne hawa ninaagiza wasimamishwe kazi, lakini wawe chini ya uangalizi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, ili kutoa ushirikiano," aliagiza.

Alisema watumishi wa umma wanatakiwa kuwa waadilifu na kuiogopa fedha ya serikali na kuahidi kuwachukulia hatua wote watakaobainika kufanya vitendo vya ubadhirifu.

Pia, aliwataka watendaji wa vijiji na kata mkoani humo kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bila kuleta 'ujanjaujanja'.

“Fedha ya serikali ni ya moto, hivyo haipaswi kulala, niwasihi tu ndugu zangu tusijaribiane, hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayehusika na upotevu wa pesa.

"Tambueni watendaji ndiyo mna dhamana ya kukusanya mapato ya ndani kutoka katika vyanzo vya mapato katika maeneo yenu," aliagiza.

Kiongozi huyo wa mkoa alisema kuna baadhi ya watumishi walikataa kusajili vyanzo vya mapato kwa makusudi na baadaye kurudi kwa wafanyabiashara na kuchukua fedha kinyemela na kusababisha serikali kukosa mapato yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live