Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aagiza walikamatwa kwa kufunga barabara Chato waachiwe

Rcpicc Data RC aagiza walikamatwa kwa kufunga barabara Chato waachiwe

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa Geita, Rosemary Senyamule amelitaka jeshi la Polisi mkoani humo kuwaachia huru watu 17 wakiwamo wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Buseresere waliokamatwa kwa tuhuma za kufunga barabara baada ya kutokea ajali ya mwanafunzi kugongwa na basi na kufariki.

Wanafunzi watano, walimu watano na wananchi saba walikamatwa Mei 9,2022.

Akizungumza na Wanafunzi na walimu wa shule hapo leo Jumatano mei 11, 2022 Senyamule amewataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi na badala yake waiache sheria ichukue mkondo wake.

"Mlijichukulia sheria mkononi kwa kufunga barabara mkaenda mbali zaidi kwa kupiga mawe magari mengine ambayo hata hayakuhusika mmevunja vioo vya magari, hii sio sawa sikuzote usikubali kufanya jambo ukiwa na hasira acheni sheria ifanye kazi"amesema Senyamule.

Mkuu huyo wa mkoa amesema dereva wa gari iliyomgonga mwanafunzi kwenye eneo la wavuka kwa miguu (zebra) anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Mkuu wa shule ya sekondari Buseresere, Mwembezi Daniel amesema shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 2000 ilikua kwenye wakati mgumu baada ya wanafunzi kuwa na mgomo baridi wakishinikiza waliokamatwa waachiwe huru.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live