Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda ameliagiza jeshi la polisi mkoani humo, kuhakikisha linamsaka afisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, ambaye anadai kuibiwa pikipiki ya serikali aliyokabidhiwa.
Amesema mtumishi huyo anatakiwa kupatikana ndani ya wiki moja ili aeleze aliibiwa katika mazingira gani pikipiki hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 1.9 na kueleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo umechukua muda mrefu bila ya kukamilika.
Amesema kupotea kwa pikipiki hiyo katika mazingira ya kutatanisha, kumesababisha kuwa moja kati ya hoja za CAG kwa halmashauri hiyo, kutokana na uchunguzi kushindwa kukamilika kwa wakati.
“RPC baada ya wiki moja aniletee taarifa ya OCD Busega juu ya upatikanaji wa pikipiki hiyo, mtumishi anayehusika atafutwe na kutoa maelezo ya kina yatakayosaidia pikipiki kupatikana, ni hii iwe onyo kwa mtumishi yeyote mwenye kifaa cha serikali kuhakikisha anakitunza,” amesema Nawanda.