Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aagiza ma-DC, wakurugenzi wasimamie ujenzi kikamilifu

4c933036d6546ec507f744bb63d2c226 RC aagiza ma-DC, wakurugenzi wasimamie ujenzi kikamilifu

Mon, 14 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametoa mwito kwa wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri na maofi sa ardhi mkoani humo wasimamie ujenzi katika maeneo yaliyopimwa ili kusiwe na ujenzi holela.

Dk Mahenge alitoa kauli hiyo baada ya kusomewa ripoti ya upimaji viwanja katika halmashauri za Mpwapwa na Chamwino wakati akiwa katika ziara kukagua miradi ambayo serikali imetoa fedha itekelezwe.

Alisema, viongozi hao wanatakiwa kuendelea na kampeni walizoanzisha za kupima viwanja, lakini wanatakiwa pia kusimamia ujenzi ili kuepusha ujenzi holela usiozingatia ramani au maelekezo ya halmashauri.

Dk Mahenge alisema hakutakuwa na maana halmashauri kugharamia kuanzisha miradi ya kupima viwanja, lakini zikaacha wananchi wajenge kiholela bila kuzingatia ramani.

Akitoa maelezo ya mradi wa upimaji viwanja Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino, Athuman Masasi alisema, halmashauri hiyo ina mkakati wa kupima viwanja 4,800 kwa lengo la kupanga mji na kuepusha ujenzi holela.

Masasi alisema halmashauri hiyo imepewa gari na vifaa vya kisasa vinavyoweza kupima viwanja 100 kwa wakati mmoja, kitendo ambacho kitaharakisha upimaji katika halmashauri hiyo.

Dk Mahenge pia alipongeza halmashauri ya Mpwapwa kwa kuanzisha mradi wa kupima viwanja vipya 1,000 katika eneo la Mazae, kata ya Mazae wiliyani humo na akaomba viongozi wa wilaya hiyo kusimamia ili ujenzi ufanyike kwa kuzingatia ramani na kuacha ujenzi holela.

“Natoa maagizo hayo kwa viongozi wote wa wilaya zote kuhakikisha kwamba pamoja na kupima viwanja hivyo, lazima kusimamia ili kuhakikisha wanajenga kwa kuzingatia ramani na kuchana na mtindo wa kujenga kiholela katika maeneo yaliyopimwa,” alisema.

Akisoma taarifa ya upimaji viwanja, Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Mpwapwa, Anderson Mwamengo alisema, halmashauri hiyo inalenga kuboresha makazi kwa wananchi wake kwa kupima viwanja katikaeneo la mazae.

Mwamengo ilisema halmashauri hiyo ina mpango wa kupima viwanja 1,000 wilayani Mpwapwa kwa lengo la kupanga mji huo ambao unakua kwa kasi na hivyo wanatakiwa kujiandaa mapema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa, Paul Sweya alisema mkakati wa halmashauri hiyo wa kupima viwanja unalenga kupanga mji, kuongeza viwanja vilivyopimwa na kukidhivi vigezo vya kuandaliwa hatimiliki.

Pia viwanja vilivyopimwa vitaongeza uwigo wa makusangto ya serikali kodi ya ardhi na majengo, kodi itokanayo na miamala ya ardhi kama vile uhamisho na rehani na kuimarisha miliki za wananchi na kuimarisha mipango ya serikali.

Chanzo: habarileo.co.tz