Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC aagiza kuondolewa kwa milango yote wodi ya wazazi

RC Aagiza Kuondolewa Kwa Milango Yote Wodi Ya Wazazi RC aagiza kuondolewa kwa milango yote wodi ya wazazi

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda ameagiza kuondolewa kwa milango yote pamoja na kufanyika kwa baadhi ya marekebisho katika ujenzi wa Mradi wa wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kijiji cha Mwaukoli Wilayani Meatu Mkoani humo.

Dkt. Nawanda ametoa maagizo hayo leo baada ya kutembelea mradi huo katika ziara yake, mradi ambao unatekelezwa na mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) ukigharimu zaidi ya Milioni 70.

Akiwa katika mradi huo, Mkuu wa Mkoa amebaini uwepo wa mapungufu mengi Katika ujenzi wa mradi huo ikiwemo fremu za milango na milango yenyewe iliyowekwa kuwa chini ya kiwango.

Mbali na hilo ameagiza kuondolewa kwa vigae viliwekwa kutokana na baadhi kukutwa vimekatika, ambapo amemwagiza Mhandisi wa Halmashauri hiyo kusimamia mradi huo kila wakati hadi kukamilika kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live