Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC: Umeme ni asilimia 100 Kilimanjaro

Umeme Tanesco RC: Umeme ni asilimia 100 Kilimanjaro

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema tangu iingie madarakani Serikali ya awamu ya sita hadi sasa mkoa huo kupitia sekta ya nishati umepokea zaidi ya shilingi Bilioni 21 kwa ajili ya kuboresha, kuunganisha na kutekeleza miradi mipya ya umeme.

Amesema usambazaji wa umeme kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umefikia asilimia mia moja Kilimanjaro mjini.

Aidha kwa upande wa vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA), usambazaji wa umeme umefikia asilimia 97.9 sawa na vijiji 508 kati ya 519 vilivyounganishiwa huduma ya umeme na vitongoji 1,911 sawa na asilimia 84.6 kati ya 2,260 ambavyo vimeunganishwa na huduma hiyo.

Babu ameongeza kuwa jumla ya wateja 68,300 wameunganishiwa umeme katika mkoa mzima wa Kilimanjaro.

Mkuu huyo wa mkoa wa Kilimanjaro ameyasema hayo wakati wa kongamano la kuangazia maendeleo ya miradi inayoendelea kutekelezwa na iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani kwa mkoa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live