Mkuu wa mkoa wa Tanga, Adam Malima ameagiza kamati ya ulinzi na usalama,wabunge na viongozi wa CCM wilaya ya Handeni kwenda kuongea na wananchi ambao wanaweka mapingamizi kwenye miradi ya maendeleo kwa madai ya kishirikina.
"Nendeni mkafanye miradi kwa wananchi wanaotaka maendeleo, hao wanaofanya mazingaombwe, mara majoka mara vitu vya ajabu ondokeni wabaki na majoka yao, watakapo amua wanataka umeme na maji watasema, na tutamuambia mama Samia, nendeni mkathibitishe na mzungumze nao, na hii michezo lazima ife" RC Tanga.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa maagizo hayo katika ziara yake ya siku moja wilayani Handeni ya kukagua miradi ya maendeleo hasa vituo vya afya na kueleza kuwa wapo wananchi wanatishia mambo ya kishirikina kwenye miradi kwa kudai fidia