Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Tabora aagiza Halmashauri kuwa na "benki za matofali"

Mkuu Wa Mkoa Tabora Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi , Dkt.Batilda Buriani

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: Michuzi blog

Mkuu wa Mkoa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameagiza Halmashauri zote kuwa na Benki ya Tofali kwa kila Kijiji.

Alisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa pindi muda wa wanafunzi wanapotakiwa kijiunga na Darasa la Kwanza ama Kidato cha Kwanza.

Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Uyui.

Alisema kutokana na maoteo ya watoto wanatakiwa kiujiunga na Darasa la Kwanza kila Mwaka ni vema kuwepo na mipango endelevu la kukabiliana na ongezeko la watoto wanaingia Kidato cha kwanza kila Mwaka.

“Hatakiwa kuwa na mipango ya zima moto ya kusubiri watoto wachaguliwe ndio tuanze kufukuzana na ujenzi wa madarasa, tuweke mipango mizuri ya kutowafanya watoto wawe wanachelewa kujiunga na masomo eti kwa sababu ya ukosefu wa vyumba vya madarsa” alisisitiza

Aliongeza kuwa sanjari na uwekaji wa mipango ya kuweka na benki ya tofali lazima kuwepo na utaratibu wa kutengeneza madawati ya kutosha ili kutowafanya wanafunzi kukaa chini.

Balozi Dkt. Batilda amesema kuwa Tabora inayo mistu ya kutoshahakuna sababu ya wanafunzi kukaa chini.Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wazazi kuweka mazingira yatakayowavutia ili walimu wapende kufanyakazi mkoani Tabora.

Chanzo: Michuzi blog