Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Songwe aagiza kuondolewa bibi afya

Songwe Pic RC Songwe aagiza kuondolewa bibi afya

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Dk. Fransisi Michael amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde kumhamisha kituo cha kazi bibi afya wa mamlaka ya mji wa Mlowo wilayani humo, Anjela Kiwale kwa kushindwa kushindwa kuwajibika na kusababisha hatari ya mlipouko wa magonjwa ya kuhara. 

Dk. Michael ametoa maagizo hayo leo Jumanne alipofanya ziara ya kushtukiza katika Soko Kuu la Mlowo na lundo la taka katika dampo zilizozagaa katika biashara za watu huku maji machafu yakitiririka katika maeneo ya baba lishe na mama lishe.

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Dk. Fransis Michael (aliyevaa kofia) akizungumza namna alivyosikitishwa na hali ya mrundikano wa taka ngumu katika soko la Mlowo wilayani Mbozi.

Amesema soko la Mlowo linawafanyabiashara wengi huku dampo lililopo likionekana wazi kuwa limezidiwa na taka nyingi ambazo zinakaa muda mrefu pasipo kuondolewa. Amesema taka hizo zimekuwa kero kubwa wananchi hasa wafanyabiashara ambapo mvua zinaponyesha maji taka yanaingia kwenye biashara zao.

”Nimepewa taarifa hizi na wasamaria wema na nimefika hapa hali ilipo hifahi, hii inaonesha watumishi idara ya afya ni wazembe, bibi afya wa eneo hili hautoshi lazima aje mtu mwngine afanye kazi hapa wewe uende kwingine’,” amesema Dk. Michael.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mlowo, Lucas Chitindi amesema hali ya uchafu katika soko hilo ni kero kubwa kwao na kwamba hukaa muda mrefu pasipo kutolewa hali inayohatarisha wananchi kupata magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde licha ya kuyapokea maagizo yaliyotolewa,  alieleza tatizo la taka kutoondolewa haraka inatokana na ukosefu wa magari kwani lipo moja pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live