Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Simiyu agawa vitambulisho vya wafanyabiashara

31164 Mtakapic TanzaniaWeb

Wed, 12 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amewakabidhi wakuu wote wa wilaya za mkoa huo vitambulisho kwa ajili ya kuwapatia wafanyabiashara wadogo.

Mtaka amegawa vitambulisho hivyo leo Jumanne Desemba 11, 2018 ikiwa si siku moja tangu Rais John Magufuli kutangaza kutoa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo na kuagiza wasibughudhiwe.

Jana jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alimkabidhi kila mkuu wa Mkoa vitambulisho 25,000  kwa ajili ya kuvisambaza katika mikoa yao kwa malipo ya Sh20,000 kila kimoja lengo likiwa ni kuwatambua wafanyabiashara hao.

Kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa facebook, Mtaka amesema amewakabidhi wakuu wa wilaya na maofisa biashara vitambulisho hivyo, kuwaagiza kuvigawa kwa wafanyabiashara ambao kwa mwaka mauzo yao ni chini ya Sh4milioni.

“Kiufupi ni wale ambao ukienda kufanya manunuzi ya 100,000 kwenye biashara yake unanunua bidhaa yote na chenji anakurudishia, wale ambao hata akiomba mkopo dhamana anaweka kitanda au viti vyake vya kukalia,” ameeleza Mtaka.

Amesema wameweka utaratibu wa kuwafuata wafanyabiashara hao walipo sambamba na kuwapa elimu wakishirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Amesema wafanyabiashara watakaotoa taarifa za uongo watanyang’anywa vitambulisho hivyo.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz