Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Sendiga "ogramu hii itamkomboa mkulima na kurahisisha utendaji kazi"

02 3 660x400 RC Sendiga "ogramu hii itamkomboa mkulima na kurahisisha utendaji kazi"

Wed, 14 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amesema, uzinduzi wa programu ya yaraConnect utasaidia serikali na wadau wa kilimo katika kufikia malengo tuliyojiwekea katika kuhakikisha wakulima wanafanya kilimo chenye tija.

RC Sendiga aliyasema hayo katika uzinduzi wa programu ya yaraConnect kwa mkoa huo mjini humo jana akisema wakulima wengi mkoani humo na kwa Tanzania kwa ujumla wanafanya kilimo cha mazoea hivyo si rahisi kuweza kuleta matokeo yenye tija.

“Ili kufanya kilimo chenye tija tunahitaji elimu na taarifa sahihi  kuhusu hali ya hewa, misimu mbalimbali ya mwaka na matumizi bora ya pembejeo za kilimo, uzinduzi huu wa programu ya yaraConnect utamkomboa mkulima na pia kurahisisha utendaji kazi wa maofisa ugani wetu ambao bado walipo hawatoshelezi” RC Sendiga

“Dunia ya sasa hivi ni dunia ya kidigitali hivyo hatuna budi kwenda sambamba na mabadiliko ya kidigitali yanayotokea, ni matumaini yetu kama serikali ya Mkoa wa Iringa na wadau wote wanaohusika tutaitumia App hii vizuri kwa malengo ya kupata ufanisi wa ili kuleta maendeleo” RC Sendiga

“Natoa wito kwa makampuni mengine ya pembejeo za kilimo kuiga mfano wa Yara kwani wamekuwa mstari wa mbele katika ubunifu ndio maana bidhaa zao zinapendwa sana na wakulima sio kwa Iringa tu bali nchi nzima” RC Sendiga

“Mkoa wa Iringa tunakuja na mapinduzi mazito sana ya kuhakikisha kuwa tunaboresha kilimo cha wananchi wa Mkoa wa Iringa na kufanya kiwe cha tija  na kuinua maisha ya wananchi wa mkoa huu hivyo mkiwa kama wadau wakubwa wa kilimo tunategemea  mtatusapoti katika kutimiza azma hii ”, RC Sendiga.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Biashara wa Yara, Andrew Ndundulu alitoa rai kwa wasambazaji wote wa bidhaa zao kuchangamkia fursa mbalimbali zanazopatikana ndani ya programu hiyo kwa kujisajili kwa wingi ili waweze kupata pointi ili kunufaika kwa kupata zawadi mbalimbali huku wakpata elimu ya utaalamu wa kilimo hivyo kuweza kuwasaidia wakulima wanaokwenda kwao kununua bidhaa za yara.



“Tunaahidi kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na uongozi wa Mkoa wa Iringa na pia tutaendela kubuni mbinu nyingine za  kidijitali zaidi ili kuhakikisha wadau wetu wanapata mafanikio mengi zaidi katika kilimo”, RC Sendiga



????????????????????????????????????
Chanzo: millardayo.com