Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Sendiga afafanua daraja lililozua taharuki Rukwa

IMG 20230406 WA0036 RC Sendiga afafanua daraja lililozua taharuki Rukwa

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga amesema video inayosambaa mitandaoni kutoka Mkoani Rukwa kuhusu Daraja la mawe linalojengwa Kalambo ina nia ya kupotosha kwakuwa bado halijakamilika na limerekodiwa likiwa bado linaendelea kujengwa na kwamba gharama za Daraja ni Tsh. Milioni 29 na sio Milioni 200 kama ilivyopotoshwa.

Queen kupitia ufafanuzi aliutoa amenukuliwa akisema; “Ukweli wa habari hii yenye nia ovu dhidi ya Juhudi ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wetu uko hivi, Daraja hili ni la upinde linajengwa Kwa mawe.



"Daraja hilo lipo katika Barabara ya Mbuluma -Lolesha - Mao ni Daraja linalojengwa na Mkandarasi aitwaye Migo lipo Kata ya Mbuluma Kijiji cha Mao kazi ilianza tarehe 24/10/2022 inategemea kuisha baadaye mwaka huu.

“Daraja linajengwa kwa kufuata taratibu za kazi lipo vizuri tu litakuwa na midomo miwili yenye kipenyo cha Mita 2.5 kila moja.



“Linavyoonekana hizo ni hatua za ujenzi likikamilika litakuwa na uwezo wa kupitisha gari lenye uzito wa Tani 30 bila shaka yeyote pia litaghalimu Tsh. Milioni 29 tu na sio Tsh milioni 200 kama Mpotoshaji alivyotaja wakati akirekodi,” amesema Queen.

Kwa mujibu wa mtu aliyerekodi na kusambaza video hiyo alkidai kuwa daraja hilo si imara limekula hela za wananchi bure na muda wowote linaweza kubomoka huku akionyesha kushangazwa na matumizi ya mbao za kuezekea nyumba wakati wa ujenzi wa daraja hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live