Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Sanare aupongeza uongozi wa Wilaya ya Ulanga

Sanare Ed.webp RC Sanare aupongeza uongozi wa Wilaya ya Ulanga

Tue, 19 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, ametoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Wilaya hiyo ikiwemo uboreshaji wa Hospitali ya Wilaya ya Ulanga.

Sanare ametoa pongezi hizo hizo baada ya kutembelea miradi miwili ya maendeleo ambayo ni ujenzi wa majengo matano ya Hospitali ya Wilaya ya Ulanga yanayojengwa kwa ufadhili wa fedha za Global Fund na ujenzi wa soko la mahenge mjini.

Amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ya ukamilishaji ya miradi hiyo na kumpongeza Mkuu wa Wilaya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na watendaji wao wote kwa usimamizi wa miradi hiyo na kuwataka wakamilishe kazi zilizobaki ili wananchi wa Mahenge waanza kupata huduma husika.

“Kwa ujumla kazi imefanyika, nikupongeza Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya kwa kusimamia kazi hii vizuri, toka niondoke sio kama nilivyoacha, ni maelekezo nilitoa wakati ule kwamba rekebisheni hapa na hapa, nimejiridhisha kazi imefanyika vizuri” amesema Sanare

Majengo matano yanayojengwa Katika Hospitali hiyo ya ya Wilaya ni pamoja na jengo la famasi, jengo la incinerator (kichomea taka), jengo la wodi ya wanaume, jengo la wodi ya wanawake, na jengp la kliniki ya macho. Majengo haya manne yamejengwa kwa gharama ya shilingi 400Mil. ikiwa ni fedha kutoka ufadhili wa global fund kupitia OR- TAMISEMI na jengo moja la macho limejengwa kwa ufadhili wa Eye Care Foundation kwa gharama ya Shilingi milioni 65.

Hata hivyo amewataka watendaji hao kuendelea kusimamia kazi zilizobaki katika miradi hiyo na kuwataka kusimamia kwa umakini mkubwa ili kutendea haki fedha zinazoletwa na serikali au wadau wengine wa maendeleo.

Wakati huohuo Sanare amewataka wafanyabiashara wa mji wa Mahenge husuani wanaojihusisha na uuzaji wa sukari, kuuza bidhaa hiyo kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali.

Ametoa maelekezo hayo baada ya kutembelea baadhi ya maduka ya Mji wa Mahenge na kubaini wafanyabiashara hao wakiuza sukari kilo moja shilingi Elfu Nne tofauti na bei iliyoelekezwa na Serikali na kuwaagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ulanga kushirikiana na Afisa Biashara na Maafisa wa TRA kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaouza Sukari kwa bei ya juu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live