Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Ruvuma awataka Watanzania kuthamini mila na desturi zao

RC Ruvuma Awataka Watanzania Kuthamini Mila Na Desturi Zao.jpeg RC Ruvuma awataka Watanzania kuthamini mila na desturi zao

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Col. Laban Elias Thomas amewataka Watanzania kuthamini mila na desturi zao ili kuvutia utalii nchini.

Col. Thomas ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya MajiMaji na Tamasha la Utalii na Utamaduni mjini Songea.

Amesema Watanzania hawatakiwi kuwa na visingizio juu ya kuthamini vya kwao na kuhamasisha utalii nchini.

"Wanzania ni lazima tuthamini vya kwetu tusiwe na visingizio bali tuone fahari" amesema Mkuu wa Mkoa.

Amesema kwa kipindi chote atakachokuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma atahakikisha kuwa wananchi wa mkoa wake wanathamini na kuonea fahari urithi walio nao.

Amewapongeza Wangoni kwa kufanya tamasha la utamaduni na utalii na kuwakumbuka mashujaa wa vita vya Majimaji kila mwaka na kuwataka makabila mengine kuiga utamaduni huo.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa urithi wa utalii na utamaduni ni tunu na unaleta umoja na amani miongoni mwa Watanzania.

Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya MajiMaji na Tamasha la Utalii hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 23 -27 Februari kwa lengo la kuwaenzi mashujaa wa vita hivyo waliouwawa na Wajerumani kwa kupinga uonevu.

Maadhimisho hayo pia yanalenga katika kuibua na kuendeleza fursa za utalii katika ukanda wa Kusini.

Maadhimisho hayo pia yanaambatana na Kongamano la Utalii litakalofanyika katika Wilaya ya Tunduru na Siku ya Wangoni inayofanyika Maposeni ambapo ni Makao Makuu ya Chiefu wa Wangoni ambapo vita vya majimaji vilianzia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live