Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Nchimbi akagua miradi ya maendeleo Manyoni

Nchimbi.webp RC Nchimbi akagua miradi ya maendeleo Manyoni

Fri, 12 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Manyoni.

Miradi aliyotembelea ni ukarabati wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya wilaya hiyo, ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata alizeti, ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari ya Kinangali, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Kinangali pamoja na kulikagua shamba la Korosho la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lenye jumla ya ekari 1,500 lililopo eneo la Sukamahela.

Akizungumza jana wakati akikagua ujenzi wa kiwanda cha kuchakata alizeti, Dk.Nchimbi aliwataka Makatibu Tawala wa mkoa huo wasikae maofisini badala yake watoke haraka waende kukagua maeneo ya uwekezaji yaliyotengwa kwenye halmashauri zao.

“RAS kwa ili tuna haja siku nyingine twende tukakague maeneo yaliyotengwa katika halmashauri zetu…taarifa za maandishi zinaeleza hayo maeneo yapo na kama yange kuwepo wewe husinge kwenda pale hukakosa hilo eneo kwa hiyo twende tuka kague hayo maeneo haraka sana.” alisema Nchimbi.

Nchimbi aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuthubutu kukijenga na kusema anaona uchumi wa wilaya hiyo utabadilika kwa sababu mzunguko wake utaenda kwa kasi yenye thamani iliyo bora kutokana na uwepo wake.

Alisema suala la mafuta ni ajenda ya kitaifa na sio ajenda binafsi ya kiwanda hicho au Manyoni na Singida, kuwepo kwake mkoa huo utachangia kuipunguzia mzigo Serikali wa kutumia fedha za kigeni kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live