Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mwanza atua walikouawa wavuvi watatu na ofisa uvuvi, awapoza wananchi

Video Archive
Wed, 24 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ukerewe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewatuliza wakazi wa kisiwa cha Siza wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza kulikotokea vifo vya watu wanne akiwemo ofisa rasilimali uvuvi wa wilaya hiyo, Ibrahim Njalali.

Mongella aliyeambatana na viongozi wengine wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo, alifika katika kisiwa hicho jana Julai 23, 2019 saa1:45 usiku na  kuzungumza na wakazi hao.

Usiku wa kuamkia jana yalitokea mauaji hayo katika mapigano kati ya wakazi wa kisiwa hicho  na maofisa wa kikosi cha kupambana na uvuvi haramu wa kanda hiyo.

Mbali na ofisa huyo,  wengine waliofariki ni Damian Joseph,  Malanja Malima na Chrisant Chrisant.  Katika tukio hilo askari polisi na mwananchi mmoja wamejeruhiwa.

Mongella amesema tukio hilo limetia doa Mkoa huo.

"Tutahakikisha haki inatendeka ili watu waliohusika na kitendo hiki waweze kuchukuliwa hatua," amesema Mongella akiwataka wananchi hao kuwa watulivu.

Pia Soma

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza,  Jumanne Muliro amesema mpaka sasa wanawashikilia watuhumiwa watatu kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Chanzo: mwananchi.co.tz