Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mwanza akoshwa na staili utendaji wa Makonda

Said Mtanda RC Mwanza akoshwa na staili ya utendaji wa Makonda

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Saidi Matanda ameeleza kuvutiwa na staili ya utendaji ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda akisema yeye anapokuwa na jambo gumu la kutolea uamuzi humuomba ushauri.

Amesema Makonda amekuwa mzoefu kwenye majukumu ya ukuu wa mkoa kwa kuwa amewahi kuongoza Jiji la Dar es Salaam na kwamba wananchi wa Arusha wamepata kiongozi kwa kuwa ni mtu wa matokeo.

“Sina shaka na utendaji wako na wakati na nimekuwa nikiiga staili yako kwa sababu unapenda matokeo na huyumbishwi. Unaweza kuanzisha jambo gumu na kuna nyakati nakuuliza unaweza kutoboa hapa, unasema bila shaka kwa sababu nafanya kwa ajili ya wananchi.

“Huwa nakufuatilia kwa karibu sana kila unachokifanya kupitia kurasa zako za mitandao ya kijamii, ukikutana na wadudu basi mimi nakuona,” amesema Mtanda baada yay eye na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu kukutana na Makonda jijini Arusha, jana Jumatatu, Aprili 29,2024

Chanzo: www.tanzaniaweb.live