Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mwanza aapa kupambana na rushwa, unyanyasaji wafanyabiashara

WhatsApp Image 2021 10 02 At 3.56.19 AM (1).jpeg RC Mwanza aapa kupambana na rushwa, unyanyasaji wafanyabiashara

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mhandisi Gabriel, ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampuni ya usafirishaji wa mizigo kutoka China,Dubai kuja Tanzania ya Silent Ocean iliyofanyika mkoani Mwanza katika  ofisi ya GSM leo.

Ameeleza kuwa mfanyabiashara atakayepata na adha hiyo taarifa ifike ofisini kwake kwani Mwanza ni sehemu sahihi ya biashara hivyo anawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kuja kuwekeza katika sekta ya Kilimo ,Biashara, Utalii, Ujenzi, Elimu, Ufugaji, na Afya.

"Serikali ya Mkoa itaendelea kuweka mazingira bora na ya haki kwa kila mfanyabiashara ili kuimarisha uwekezaji na kuhamasisha katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii hivyo kampuni hii ya usafirishaji  mfanye kazi kwa uaminifu ili kuwajengea amani wafanyabiashara" ameeleza Gabriel.

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo ,Mohamed Soloka amesema kuwa wameamua kufungua tawi mkoani Mwanza kutokana na uhitaji mkubwa wa wafanyabiashara waliokuwa wakifuata mzigo dar es Salam hivyo wamewaondolea adha hiyo.

Ameongeza kuwa mizigo yote itasafirishwa katika hali nzuri hivyo ni wakati wa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo pia njia hiyo itaongeza  pato la serikali kupitia kodi kutokana endapo wajasiliamali wataongezeka .

Naye mkuu wa Masoko na mauzo, Mohamed Kamilagwa amesema itawapunguzia Wafanyabiashara usumbufu wa kusafirisha biashara kutoka China na Dubai kuja Mwanza hivyo kunufaika kiuchumi.

“Mteja atasaidiwa kupunguza usumbufu wa kuulizia mzigo kutoka Dar es salaam lakini wale wajasilimiamali  tulionao itawarahisishia kuwapunguzia gharama za kusafirisha ,usumbufu wa kuuliza na kuokoa mda ,”amesema Kamilagwa.

Chanzo: ippmedia.com