Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mtwara awaonya wakurugenzi waliokimbia kikao

Rc Ed.jpeg RC Mtwara awaonya wakurugenzi waliokimbia kikao

Wed, 12 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Byakanwa ametoa kauli hiyo leo, wakati akifungua kikao hicho cha mkoa kilichokuwa na lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe kuanzia julai 2020 hadi Desemba 2020.

Amesema ni jambo la kusikitisha kuona kikao hicho muhimu kinakosa watoa maamuzi na washauri wa masuala ya lishe katika wilaya zao na badala yake wametuma wawakilishi.

“Kwa wakurugenzi na wakuu wa mipango miji ambao hawajafika waliotumwa kuwawakilisha kila anayesimama anasema aliyemtuma anaumwa sasa nakuagiza RAS ikifika tarehe 13 kesho kutwa nipate taarifa ya kila mmoja mezani kwangu, kama walikuwa wanaumwa na walienda kutibiwa wapi, lakini jambo hili linasikitisha zaidi kuona hata wakuu wa wilaya waliohudhuria hawana taarifa za watu wao waliotuma wawakilishi” amesema Byakanwa.

Wakurugenzi walioshindwa kuhudhuria kikao hicho wanatoka katika Halmashauri za  Nanyumbu,Nanyamba Mtwara na Masasi ,ambapo kati ya hao  mkurugenzi wa halmashauri ya Masasi pekee ndiyo taarifa za kutokuwepo kwake zilimfikia Kaimu katibu tawala.

Amesema alichobaini baada ya watendaji wengi wa mkoa huo kushindwa kuhudhuria kikao hicho pasipo kutoa taarifa kwa ngazi husika kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kutojua misingi ya uongozi na mifumo yake ya mawasiliano.

“Kilichotokea leo,kwa sisi kushindwa kupeana taarifa kinaonyesha wazi umuhimu wa kupata semina elekezi juu ya nafasi zetu na kwa bahati mbaya sana kwa muda wa miaka mitano iliyopita mafunzo haya hayakufanyika watu walikuwa wanateuliwa na kuingia kwenye majikumu bila ya kupata mafunzo yoyote ya uongozi” amesema Byakanwa.

Akizungumzia tathmini hiyo ya afua za lishe Byakanwa , amesema mkoa wa Mtwara usijifungie katika tathmini yap eke yake bali walinganishe na mikoa mingine kwa ajili ya kujua wapi wamefanya vizuri na wapi wamekosea kwa ajili ya kutilia mkazo maeneo yenye upungufu.

“Tunapotekeleza na kujadili tathmini zetu tujilinganishe na mikoa mingine wao wamefanyaje tuangalie mapungufu yetu  wapi tumefanya vibaya na wapi tunahitaji kuongeza nguvu” amesema Byakanwa.

Kuhusu athari za lishe kwa watoto Byakanwa, amesema suala hilo lisipotiliwa mkazo vya  kutosha jamii itatikisika kiuchumi kwa kile alichoeleza athari hizo ni pamoja na kukosekana nguvu kazi kwa wakati ujao, pamoja na kuwa na kizazi chenye mtindio wa ubongo kwa asilimia kubwa.

Amesema kinachochangia hali ya utekelezaji wa afua za lishe kushindwa kufikia malengo kwa asilimia mia licha ya bajeti yake kutengwa ni pamoja na fedha husika kutofikishwa kwa walengwa waliokusudiwa.

Awali mganga mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dk Silvia Mamkwe, alisema malengo ya tathmini hiyo ni kuangalia namna ya kupunguza hali ya utapiamlo katika mkoa huo na kuboresha hali ya lishe kuanzia ngazi ya kijiji kwa ajili ya kuwa na jamii bora.

Chanzo: ippmedia.com