Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mtwara atoa saa 48 kukamilika madarasa 452

Mtwara Pic Data RC Mtwara atoa saa 48 kukamilika madarasa 452

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza Halmashauri zote mkoani humo kukamilisha majengo 452 ya madarasa ndani ya saa 48.

Madarasa hayo 452 yamejenga na fedha za Uviko-19 na yapo katika hatua ya umaliziaji.

Akizungumza leo Jumanne Desemba 7, 2021 wakati wa kupokea vyumba vya madarsa 22 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya, Gaguti amesema kuwa Halmashauri zote zinatakiwa kufanyakazi usiku na mchana ili kukamilisha madarasa hayo ndani ya saa 48.

Amesema kuwa madarasa hayo yanajengwa kwa fedha za Uviko-19 ambapo kwa Manispaa ya Mtwara Mikindani ampokea madarasa 22 yenye thamani ya Sh440 milioni.

"Nataka hadi kufikia Desemba 10 mwaka huu madarasa 452 yenye thamani ya Sh11.67 bilioni yawe tayari nimekabidhiwa fanyani kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo" ameagiza Gaguti

"Tuendelee kujenga majengo yetu kwa kasi hii hii ni dhambi kwa watumishi kupewa fedha za ujenzi wa miradi na kushindwa kukamilisha kwa wakati tunakuwa hatutendi haki kwa wananchi na Serikali pia"

Advertisement "Tunazo zaidi ya Sh11 bilioni kwenye miradi ya afya na elimu nataka ikamilike kwa wakati ili shughuli zingine za maendeleo ziweze kufanyika ingawa kwa leo nakagua madarasa" amesema

Chanzo: www.mwananchi.co.tz