Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mtaka awaka: Nawapa siku saba waliodai fidia kwa udanganyifu

A2fed60d A6e1 4fb3 B502 2f23673588c3 768x512 RC Mtaka awaka: Nawapa siku saba waliodai fidia kwa udanganyifu

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, amewataka Wananchi Mkoani Dodoma waliovamia maeneo ambayo Serikali imetwaa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kitaifa na kujirodhesha kudai fidia katika uwanja wa Ndege wa Msalato kwa njia ya udanganyifu, kufika katika ofisi za mtaa kuondoa majina yao haraka.

Hayo ameyasema hayo jana Julai 22,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi wa mkoa pamoja na watumishi idara ya ardhi kuhusu tamko kuhusiana na madai ya viwanja vya Msalato.

Amesema kwa mujibu wa sheria ya kanuni za Adhabu sura ya 16 toleo la 2019,kifungu 301 na 302 ni kosa la jinai kufanya udanganyifu kwa lengo la kujipatia fedha za serikali, adhabu ya hatia hii ni jela miaka 7, sambamba na jela kwa mujibu wa kifungu cha 31 sura ya 16 toleo la 2019, Mahakama yaweza kukuamuru ulipe fidia kwa madhara uliosababisha kwa Serikali kupitia udanganyifu wako.

“Ninatoa siku saba kuanzia leo tarehe 22 Julai, 2 hadi 29 Julai, 2022 kuondoa majina ndani ya siku hizo bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria,"amesema.

“Watakaokaidi wito huu timu yangu itafanya msako mkali kubaini wanaodanganya kwa nia ya kujipatia fidia isiyo halali na kuingiza serikali hasara watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungwa jela miaka saba,” amesema Mtaka.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amesisitiza wanunuzi wa ardhi wa Jiji la Dodoma watambue mamlaka ya upangaji ni mkurugenzi wa Dodoma, kwa mujibu wa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi.

“Ni muhimu kujiridhisha eneo ambalo unalinunua tena ukiwa na mkurugenzi wa Dodoma kinyume cha hapo utajiingiza kwenye migogoro na susi serimali unatutia kwenye changamoto hiyo”,amesema

“Tumekuwa tukichukua hatua kwa watumishi wa umma na wako watumishi wamesimamishwa kazi na bado wapo mitaani na pia wale wanaowasababishia watumishi wetu kuingia kwenye ulaghai tumeshawachukulia hatua”.Amesema Shekimweri

Naye Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga,amesema Serikali inakumbukumbu kwa kila mtu aliyelipwa fidia hivyo kuwa makini katika suala la kutaka kulipwa fidia kwa kugeuza majina

“Serikali ilianza kulipa fidia kutoa eneo kujenga uwanja wa kimataifa tangu 2008 na Baadhi ya Wananchi walilalamika hawakulipwa fidia na hapo Serikali ilisikia na 2012 na 2019 Ilitoa tena fedha nyingi kulipa fidia, lakini sahivi kuna wimbi kubwa la watu limejitokeza kutaka kulipwa fidia”,amesema

“tunaomba sana kama umetumia njia aramu ya kuomba fidia naomba futa jina mapema tumtii Kiongozi wetu wa mkoa ili tuendelee na shughuli nyingine za kimaendeleo Mkoani kwetu,” amesema Mganga.

Naye Kamishna wa Ardhi Jiji la Dodoma, Thadei Aldo Kabonge amesema sheria itachukua mkondo wake kwa wale wasio waaminifu katika kukiuka sheria na taratibu zilizopangwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live