Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mtaka atoa neno mikopo ya wanawake

Mtakapic Data Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Tanzania, Anthony Mtaka amewataka viongozi wa halmashauri kuwa wabunifu katika mikopo inayotolewa kwa wanawake, vijana na walemavu ili tija yake iweze kuonekana katika fedha hizo.

Akizungumza katika kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC), Mtaka amesema yeye sio muumini wa watu kugawiwa fedha katika mfumo huo wa mikopo.

“Mimi sio muumini wa kuwapa watu fedha kwa sababu Mungu ametupa akili, ametupa maarifa. Ndio maana Mafuru (Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru) wakati unakabidhi (mikopo) mimi sikuja.

“Unawapa Sh1 bilioni mwaka jana ulitoa Sh4 bilioni lakini katika watu ambao unawatoza ushuru hawana uhusiano na vile vikundi,”amesema.

Amesema kuna watu walio na mtaji kidogo wa biashara lakini wamekuwa wakikuwa kibiashara.

Amehoji kwanini wasiweke mazingira tofauti kwa kuwa na ruzuku ambayo makundi hayo yatashindania kwa kuandika andiko la biashara kuna majiji yenzako yanapata.

“Basi tu kwasababu ni siasa tusigombane na watu lakini model (mfumo) hii kama utaenda kuimplement (kuitekeleza) utaona matokeo yake,”amesema.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi, Donald Mejitii amesema Serikali imelenga kutenga na kutoa mikopo ya asilimia 10 tu hakuna msisitizo wa kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa ili kuwepo na mzunguko.

“Tumejielekeza kutenga asilimia 10. Hakuna lugha inayosemwa kuwa wale waliokopeshwa warejeshe mikopo na sheria haikusema hao walipokopeshwa warejeshe,”amesema.

Ametaka viongozi kuacha kujipendekeza kwa wananchi na badala yake kuwaambia ukweli kuwa fedha hizo zinatakiwa kurudishwa sambamba na kuweka utaratibu utakaowafanya kuzirejesha.

Amesema mtu anapewa mkopo wa Sh5 milioni lakini mwisho wa siku anaishia kurejesha Sh400,000

Mejitii ameshauri wafanyabiashara kujengewa uwezo utakaowezesha kukopa na kulipa ili waweze kukopesheka na taasisi nyingine za kifedha.

Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mafuta mkoani hapa Deus Nyabiri amesema inabidi kwenda mbali kabla ya kuwakopesha watu hao kwa kuchukua wale wenye biashara.

Amesema ukichukua mtu ambaye hajawahi kufanya biashara inabidi umfundishe biashara na kwamba hoja sio kiasi ni kidogo wanachopewa bali ni uwezo wa mtu kibiashara.

“Kuwajengea knowledge (uelewa) wa kurudishwa. Hawa hatuwaandai sawasawa tuwawekee riba ndogo,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live