Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Morogoro ataka soko lijengwe usiku na mchana

34806 Pic+soko Tanzania Web Photo

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe ameiagiza kampuni inayojenga Soko Kuu la Manispaa ya Morogoro kufanya kazi ya ujenzi huo usiku na mchana.

Amesema inapaswa kufanya hivyo ili kufidia muda watakaoupoteza zitakapoanza mvua za masika.

Ametoa agizo hilo leo Januari 4, 2018 alipofanya ziara katika soko hilo akiambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ili kujiridhisha na maendeleo ya ujenzi huo.

Amesema ujenzi wa soko hilo upo nyuma ya ratiba iliyopangwa na kutaka ufanyike usiku na mchana.

 “Baada ya kuona kuna uchelewaji nimewaelekeza wajenge usiku na mchana ili hata kama ikitokea bahati mbaya mvua zitakuja kwa wingi wawe wamekwisha okoa sehemu ya muda,” amesema Dkt. Kebwe.

Meya wa manispaa ya Morogoro,  Pascal Kihanga amewatoa hofu wafanyabiashara wa manispaa hiyo kutekeleza makubaliano waliyokubaliana awali wakati wa kuondoka kupisha ujenzi wa soko hilo.

Msimamizi wa ujenzi wa soko hilo, Antonio Mkinga ametaja changamoto za mradi kuwa ni pamoja na eneo la mradi kuwa kwenye bonde na kuwa jirani na Mto Kikundi jambo alilodai kuwa linaathiri mwenendo wa ujenzi.



Chanzo: mwananchi.co.tz