Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mongella ataka wamachinga kupelekwa maeneo rafiki

82279 Pic+mongela RC Mongella ataka wamachinga kupelekwa maeneo rafiki

Wed, 30 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza.  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  John Mongella amewataka wakurugenzi watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya Jiji  la Mwanza kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika mifereji ya kupitisha maji.

Mongela amewaeleza John Wanga (Ilemela) na Kiomoni Kibamba  wa Halmashauri ya Jiji leo Jumatano  Oktoba 30, 2019 katika kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mkoani Mwanza.

Amesema wafanyabiashara wadogo wametumia uhuru waliopewa na Rais John Magufuli kupitiliza na kuanza ujenzi wa vibanda katika mifereji ya maji mbele ya nyumba za watu kitu ambacho sio sahihi.

“Sasa hivi ndugu zetu wale si kwamba ni wamachinga tena, ni wafanyabiashara wakubwa unakuta mtu kajenga duka kwa kutumia grili na mabati na kuchomelea.”

“Na utakuta nyuma yake kuna duka ambalo mmiliki wake analipa ushuru, ana leseni ya biashara na analipa kodi TRA, hapa ni kama tunajipiga risasi mkononi,” amesema Mongella.

Amesema wakurugenzi hao wanatumia kigezo cha uchaguzi wa Serikali za mitaa kutoshughulikia suala hilo, kuwataka kutumia kipindi hiki kuwataka wafanyabiashara kuhama maeneo ya pembezoni  mwa barabara na kwenye mifereji.

Chanzo: mwananchi.co.tz