Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mongella ataja faida ujenzi wa Meli mpya, Chelezo

87607 Pic+mongela RC Mongella ataja faida ujenzi wa Meli mpya, Chelezo

Thu, 12 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Utekelezaji wa miradi, hasa ile mikubwa huambatana na mambo na faida kadhaa kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa eneo la mradi.

Hivyo ndivyo ilivyo pia kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, hasa jiji la Mwanza nchini ambako utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli mbili unatekelezwa.

Miradi hiyo ni ujenzi wa meli mpya ya Mv Mwanza Hapa Kazi Tu kwa gharama ya zaidi ya Sh89 bilioni, Chelezo kitakachogharimu Sh36 bilioni.

Serikali pia inafanya ukarabati mkubwa wa meli ya Mv Victoria kwa gharama ya Sh22.7 bilioni pamoja na Mv Butiama inayokarabatiwa kwa Sh4.9 bilioni.

Akizungumza jijini Mwanza leo Jumapili Desemba 8, 2019 wakati wa hafla ya kuweka mawe ya msingi ya miradi hiyo inayotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh152 bilioni, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ametaja faida nne zinazoambatana na miradi hiyo.

Akitoa salaam za mkoa mbele ya Rais John Magufuli, mkuu huyo wa mkoa ametaja faida hizo kuwa ni fursa za ajira kwa Watanzania, biashara, muingiliano na mahusiano kati ya Watanzania na wataalam kutoka nje wanaotekekleza miradi hiyo.

“Faida nyingine ni mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana na wataalam wa Tanzania kuhusu teknolojia mpya nay a kisasa ya ujenzi wa meli,” amesema Mongella

Meli mpya inajengwa na kampuni ya Gas Entec akishirikiana na KANG NAM zote kutoka Korea ya Kusini ambao wanashirikiana na SUMA JKT ya Tanzania.

Chelezo inajengwa na kampuni ya ukandarasi ya Stx Engine inayoshirikiana na SAE KYUNG zote za nchini Korea ya Kusini huku ukarabati wa Mv Victoria na Mv Butiama zinakarabatiwa na kampuni ya KTMI pia ya nchini Korea ya Kusini.

Chanzo: mwananchi.co.tz