Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mongella ahoji mhubiri Zumaridi kujiita Mungu

82498 Mhubri+pic RC Mongella ahoji mhubiri Zumaridi kujiita Mungu

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  John Mongela ameshangazwa na mhubiri Zumaridi kujiita Mfalme Mungu, kuhoji sababu za kiongozi huyo wa dini kujiita Mungu.

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 31, 2019 katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Mwanza, Mongella amesema kuabudu ni haki ya kila mmoja ila Serikali haiko tayari kuona dini inayotatanisha na kuhatarisha usalama wa jamii.

"Hakuna dhehebu linalosema kuwa kiongozi wa dhehebu hilo ndio Mungu. Madhehebu yanakuwa na viongozi lakini wanamuomba Mungu, sasa huyu Mfalme Zumaridi ninamshangaa.”

"Nimesema hili humu ili kama kuna muumini wake apeleke taarifa ili wakae na kujadili kuhusu suala hili haiwezekani kiongozi wa dini anawalaza waumini na kuwafanya kama sakafu kwa kupita juu yao,  hii inahatarisha usalama wao,” amesema Mongella.

Chanzo: mwananchi.co.tz