Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mnyeti awarejeshea tabasamu wananchi walioporwa ekari 1,000 za ardhi

98281 Pic+mnyeti RC Mnyeti awarejeshea tabasamu wananchi walioporwa ekari 1,000 za ardhi

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro. Wakazi wa kijiji cha Landanai kata ya Naberera wilayani Simanjiro wameshukuru Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti kwa kuwapatia ekari 1,000 za ardhi zilizoporwa na kigogo mmoja wa wilayani humo.

Wakizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Machi 7, 2020  wakazi hao wamedai kuwa uamuzi huo wa Mnyeti  ni ushindi kwao.

Julius Ezekiel amesema ardhi yao ilichukuliwa na mafisadi wa ardhi na wao wakalalamikia jambo hilo kwa Mnyeti kuagiza warejeshewe.

Amesema kigogo mmoja wa wilaya hiyo aliwapora ekari na wakakosa a sehemu ya kuchungia mifugo na kulima kutokana na tamaa ya mtu mmoja.

Diwani wa Naberera, Haiyo Mamasita amemshukuru mkuu huyo wa mkoa kwa hatua hiyo, "huyo kigogo alitumia nafasi yake ya udiwani na kujimegea ardhi hiyo ekari 1,000 bila uhalali na sisi tulipodai alitumia nafasi yake kung’ang’ania eneo hilo.”

Mnyeti amesema alifanya ziara ya kuzungumza na wananchi hao mwishoni mwa mwaka jana na wakamueleza tatizo hilo.

Pia Soma

Advertisement
"Baada ya kuunda kamati ya kufuatilia suala hilo tulibaini kuwa wananchi wana haki huyo mmiliki hakupewa kihalali ndipo nikaagiza wananchi warudishiwe eneo lao," amesema Mnyeti.

Amesema ameshatoa maelekezo juu ya matumizi ya ardhi ekari 1,000 hivyo irudishwe kwa wananchi hao ambao watapanga matumizi ya eneo hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz