Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mndeme akabidhi gari la wagonjwa kituo cha afya Mapera

Ambulance Ruv Ed.webp RC Mndeme akabidhi gari la wagonjwa kituo cha afya Mapera

Tue, 16 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, amekabidhi gari la kisasa la kubebea wagonjwa (Ambulance) katika Kituo cha Afya Mapera kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambalo limenunuliwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 138.

Akitoa taarifa kabla ya uzinduzi na makabidhiano ya gari hilo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Juma Mnwele, amesema wamefanikiwa kununua gari hilo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Mnwele amesema, gari hilo la wagonjwa limekatiwa Bima kubwa (Premium) ya Shilingi Milioni 6.3 na kwamba limepangiwa kutoa huduma za rufaa kwa wanawake,watoto na wagonjwa wengine katika kituo cha Afya cha Mapera ambacho kimejengwa kwa fedha za serikali kilichoghalimu kiasi cha shilingi milioni 400.

“Sisi watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga,tunaona fahari na faraja kuungana na Mhe.Rais John Magufuli ambaye alituletea milioni 400 za kujenga kituo cha afya Mapera na Halmashauri tumenunua gari la wagonjwa ,yawezekana haijawahi kufanyika mahala pengine’’,amesema Mnwele.

Akizungumza kabla ya uzinduzi na kabla ya kukabidhi gari hilo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Mbinga kwa kuweza kununua gari la wagonjwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Mndeme amesema Kituo cha afya Mapera ni kati ya vituo vya afya 16 vipya ambavyo vinajengwa katika Mkoa huo kutokana na fedha ambazo zimetolewa na Rais John Magufuli kwa lengo la kuboresha afya kwa wananchi wake.

Hata hivyo Mndeme amesema katika Halmashauri za Mkoa huo, ujenzi wa Hospitali nne za Wilaya unaendelea kutekelezwa na kwamba serikali imedhamiria kuona Taifa na wananchi wanakuwa na afya bora ili waweze kutekeleza majukumu yao.

“Ninyi wananchi wa Mbinga kwa namna ya kipekee mmeamua kutumia fedha zenu za mapato ya ndani kununua ambulance ili kumuunga mkono Mhe.Rais wetu katika juhudi za kuboresha sekta ya afya kwa wananchi’’ amesisitiza Mndeme.

Serikali imeajiri madaktari wapya 24 katika Mkoa wa Ruvuma ambao wamepangiwa kufanya kazi katika vituo vya afya na hospitali,ikiwemo madaktari wawili ambao wamepangiwa katika kituo cha afya Mapera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live