Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC: Mnaowapa wanafunzi mimba tutawanasa

Mimba Wanafuzi RC: Mnaowapa wanafunzi mimba tutawanasa

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache tangu ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan autaje Mkoa wa Songwe kuwa unaongoza kwa mimba za utotoni, Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Francis Michael ameliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Walimu kuhakikisha Wanaume wanaosababisha mimba za utotoni katika Mkoa huo wanakamatwa.

Dkt. Michael amesema “Nashukuru Mkoa wetu haukutajwa kwenye udumavu, ingawa unaongoza kwa jambo moja mmesikia juzi jambo baya sana, wote tushikane mikono pamoja tukapambane na mimba za utotoni, Rais amesema tukalifanyie kazi, Askari mna nafasi kubwa sana, Walimu Mashuleni mnatakiwa mtuambie Mtoto akiacha Shule kwa sababu ya mimba lazima tuwe tunampata Mhusika, hawa Wajinga wanaotuharibia Watoto lazima tuwakamate”

Itakumbukwa October 28,2023 wakati Rais Samia akipokea Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto ya Mwaka 2022, alisema ripoti hiyo inaonesha Mkoa wa Songwe una kiwango kikubwa cha mimba za utotoni ukilinganisha na Mkoa mwingine wowote Tanzania.

Katika ripoti hiyo Mikoa inayoongoza kuwa na kiwango kikubwa cha mimba za utotoni ni Songwe (45%), Ruvuma (37%), Katavi (34%), Mara (31%) na Rukwa (30).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live