Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mjema atoa mbinu hii kupata fedha

Mjema Pic Data RC Mjema atoa mbinu hii kupata fedha

Wed, 26 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (RC), Sophia Mjema amewataka vijana na kina mama wa Manispaa ya Shinyanga kuchangamkia fursa ya mradi wa kuchakata tope kinyesi ili waweze kupata fedha.

Mjema ametoa wito huo leo Jumatano Januari 26, 2022 wakati akizindua mradi wa bwawa la kuchakata maji taka katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga, uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo SNV kutoka Uholanzi, ambao utasaidia vijana kujiajiri na kujiongezea kipato.

Amesema baadhi ya vijana wamekuwa wakijitafutie fedha kwa kufanya maovu lakini kwa sasa fursa ya kupata fedha imepatikana wanatakiwa wapate mafunzo na watengeneze mbolea, nishati mbadala na gesi waweze kujipatia fedha ya halali.

"Kuanzishwa mradi huu ni fursa kwa wananchi wa Shinyanga mnatakiwa mjiongeze, kinyesi hiki mnachokiona ni mali na ni dhahabu. Vijana na kina mama changamkieni fursa hii ili muweze kujikwamua na umasikini" amesema Mjema.

"Nawaomba sana wataalamu wote mliopo hapa mtoe mafunzo kwa wananchi wanaohitaji kupata mafunzo haya ili waweze kujiongezea kipato na kuondokana na umasikini, acheni mambo ya kujipatia fedha kwa kufanya maovu njoni mjipatie fedha kwenye mradi huu".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shuwasa, Mwanvua Jilumbi amesema kabla ya mradi huo uzoaji majitaka ulikuwa ukifanyika kiholela na kusababisha magonjwa ya milipuko lakini kwa sasa bwawa hilo litasaidia kumwaga maji taka na yatachakatwa kikamilifu.

Advertisement "Nalishukuru sana Shirika la Maendeleo SNVĀ  la Uholanzi kwa kutuletea mradi huu wa kuchakata maji taka, hivyo tutaendelea kuutunza na tunajiandaa kwa awamu ya pili ili kuufikia uchumi wa kati, tunawashukuru wananchi kwa kutupatia eneo hili ambalo ni heka mbili"amesema Jilumbi.

Naye Balozi wa Tanzania kutoka Uholanzi, Wiebe Deboer amesema mradi huo umetumia Sh310 milioni mpaka kukamilika.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Masumbuko amesema mradi huo umeonekana kuwa na manufaa mengi, kwani kutoa kinyesi ni suala zuri sana katika mazingira, hivyo itasaidia kuondokana na magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na kinyesi.

Mradi huo uliozinduliwa leo umefadhiliwa na Shirika la maendeleo SNV kutoka Uholanzi unasimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Shinyanga (Shuwasa)

Chanzo: www.mwananchi.co.tz