Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mgunda awapongeza CRDB kuwakopesha wakandarasi wazawa

Capture22 RC Mgunda awapongeza CRDB kuwakopesha wakandarasi wazawa

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba amezitaka Taasisi za kifedha nchi kuendelea kuwakopesha Wakandarasi Wazawa ili waweze kutekeleza miradi yao kwa wakati.

Wito huo ameutoa wakati wa semina kwa wateja wa Bank ya CRDB iliyofanyika mjini Tanga na kuhudhuriwa na wateja zaidi ya 1000.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa miongoni mwa wafanyabishara na Wakandarasi wengi walikuwa wanakosa kazi na wengine kazi zao zilikuwa zinasuasua kutokana na ukosefu wa mitaji. Alisema kwamba mashariti ya Serikali kuwapa kazi ni lazima wawe na fedha ya kuanzia kutekeleza mradi huo.

Mgumba alieleza kwamba wengi waliokuwa na mitaji midogo walikuwa hawetekelezi kwa wakati na miradi mingi ilikuwa inachelewa.

“Nawapongeza Bank ya CRDB kwa kuamua kuwapa mikopo wakandarasi wakubwa hadi sh.billion 20 na pia wakandarasi wanaweza kuungana watano au kumi wakapewa mitaji ya kutosha kitu ambacho kimeondoa changamoto hiyo ya mitaji, " amesema Mgumba

Mkuu huyo wa Mkoa amesema pia bank hiyo mwanzo ilikuwa inawapa wajasiriamali wadogo kama vile mama lishe, baba lishe na wafanyabishara wa sokoni mikopo ya sh.50 million. Sasa hivi, amesema, wameongeza hadi sh 2 billion.

Pia amesema kuwa katika bajeti hii inayoendelea r Serikali imetenga bajeti ya sh trillion 3.8 kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi na kati ya hiyo Sh tillion 1.4 ni kwa ajili ya sekta ya ujenzi hivyo fedha ya kuwalipa wakandarasi watakaopata kazi kwenye miradi kwenye barabara na kwenye viwanja vya ndege na mingine yote fedha za kuwalipa zizo. Aliitaka bank ya CRDB iendelee kuwakopesha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Abbdulmajid Nsekela alileza kuwa Benki hiyo imeandaa semina hiyo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili kuwaleleza fursa zilizopo ikiwepo pamija na uoanuzi wa Bandari ya Tanga na bomba la Mafuta.

Amesema upanuzi wa bandari utasababisha kuogeza kwa mizigo inayopakuliwa na kusarifisha kupitia bandari ya Tanga jambo ambalo ni fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali.

Mkurugenzi huyo pia amesema kuwa benki imeanzisha bidhaa nyingine inayoitwa mbegu ambayo inawalenga wajasirimali wanawake na vijana mabo wana mawazo ya ubunifu ambapo watapatiwa mitaji(mikopo) kwa ajili yakuendeleza mawazo na biashara zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live