Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mbeya aagiza jengo la abiria Songwe likamilike

Homera Web RC Mbeya aagiza jengo la abiria Songwe likamilike

Sat, 24 Dec 2022 Chanzo: eatv.tv

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera, amemwagiza Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe (SIA), kukamilisha mradi huo ifikapo mwezi Februari mwakani.

Homera ametoa  maagizo hayo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa walipotembea na kukagua ujenzi wa mradi huo unaogharimu zaidi ya bilioni 33.

Homera amesema kukamilika kwa jengo la abiria, kutafungua fursa za kiuchumi mkoani humo na  kushauri kujengwa kwa zahanati katika eneo hilo ili kusaidia upatikanaji wa huduma za afya kwa  watumiaji wa uwanja huo pale itakapotokea dharura.

Kwa upande wake Meneja wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mbeya Mhandisi Matari Masige amesema asilimia 95 ya matengenezo ya uwanja yamekamilika na kuahidi kamalizia sehemu iliyobaki ndani ya muda uliopangwa.

 

Chanzo: eatv.tv