Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Masenza awasihi wanaume wapime VVU

11997 Vvu+pic TanzaniaWeb

Mon, 23 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amewataka wanaume kujitokeza kupima maambukizi ya virusi vya Ukimwi ili kutambua kama wameambukizwa.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuacha tabia ya kujificha nyuma ya migongo ya wanawake hali anayoitaja kuwa haitoi picha halisi ya maambukizi kwa wahusika.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Julai 23, 2018 Masenza amesema wapo wanaume ambao kwa kukosa ujasiri wa kujitokeza kupima hali yao ya maambukizi ya VVU hutumia matokeo ya vipimo vya wake zao ama wapenzi.

"Takwimu nyingi zinaonyesha wanawake ndio wanapima ukimwi kuliko wanaume na hii ni kutokana na wanaume kushindwa kujitokeza na kudhani mkewe akipima na yeye tayari kapima, hii sio sahihi ni vyema kila mtu akipima vipimo vyake" amesema Masenza

Amesema kwa kutambua hali hiyo Serikali imeamua kuwahamasisha wanaume wajitokeze kupima kutambua hali yao huku akitoa changamoto kwenye takwimu za hivi karibuni za maambukizi ya VVU katika mkoa huo zinazoonyesha ongezeko la maambukizi mapya kufikia asilimia 11.3.

Kwa upande wake, Kaimu Mratibu wa tume ya kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa, Dk Chrisantius Ngowi amesema kwa sasa nchi inauwezo wa kuwahudumia watu wenye maambukizi ya VVU hivyo kuwaomba watu wote kujitokeze kupima

Kampeni ya “FURAHA YANGU, PIMA, JITAMBUE, ISHI” ilizinduliwa hivi katibuni na Waziri mkuu Kasimu Majaliwa ikiwa ni kampeni ya nchi nzima katika kuhakikisha kila mtu anapima afya yake na kujitambua.

Chanzo: mwananchi.co.tz