Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Marco Gaguti amekutana na uongozi wa Dangote Mtwara

2826bf1712b8c5bfe84df556768ac5d0 RC Marco Gaguti amekutana na uongozi wa Dangote Mtwara

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Generali Marco Gaguti amepongeza Uongozi wa Kiwanda cha Saruji Cha Dangote kwa kuongeza uzalishaji wa saruji itakayosafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara kwenda Dar es Salaam na maeneo mengine nchini.

Generali Gaguti ametembelea kiwanda hicho kuona hali ya uzalishaji wa saruji na kufurahishwa na hatua za hizo zenye lengo la kutoa fursa katika bandari hiyo kwa kusafirisha kwa urahisi.

“Dangote anatumia Bandari ya Mtwara kupeleka saruji Zanzibar na Comoro, sasa wana mpango wa kuzalisha saruji kwa kiwango kikubwa zaidi na kutumia bandari yetu,” amesema Generali Gaguti.

Aidha, Uongozi wa kiwanda hicho umepanga kuongeza kiwango cha uzalishiji wa saruji, kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho, Abdullahi Baba.

Abdullahi Baba amesema uzalishaji wa saruji umeongezeka na kufikia tani milioni 1.8 kwa mwaka huu. Amesema wamepanga kuongeza kufikia tani milioni 2 ifikapo 2022.

Chanzo: www.habarileo.co.tz