Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Malima ataja wabunge watatu Mwanza wanaomnyima usingizi

RC Malima Atoa Siku 7 Walioua Albino Wakamatwe RC Malima

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adamu Malima amewataJa wabunge watatu, Hamis Tabasamu (Sengerema),  Eric Shigongo (Buchosa) pamoja na Alexander Mnyeti (Misungwi) kuwa ni wabunge wanaomnyima usizingizi wanapotaka kusukuma masuala ya maendeleo kwenye majimbo yao mkoani hapa.

Kauli hiyo ameitoa jana Jumapili Aprili 23, 2023 kwenye hafla ya utiaji saini ujenzi wa Barabara ya Lami ya  Sengerema -Nyehunge yenye urefu wa km54.4 ambayo itajengwa kwa fedha za ndani kwa gharama ya Sh73.04 bilioni ambayo inatarajiwa kukamilika ndani miaka miwili.

Malima amesema wabunge hao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wa majimbo yao wanapata maendeleo ambapo kwa sasa mchakato wa ujenzi wa barabara ya Sengerema -Nyehunge umekamika na utapunguza usumbufu kwa wabunge hao.

Kwa upande wake, mbunge wa jimbo la Misungwi, Alexander Mnyeti ametishia kushikilia shilingi bungeni Kama barabara ya Misasi-salawe-Kahama haitawekwa kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami.

"Nakuomba Waziri wa ujenzi na uchukuzi kama barabara ya Misasi hadi salawe hadi Kahama haitaingizwa kwenye mpango wa kujengwa kwa lami sitakuwa tayari Kupitisha Bajeti hiyo,” amesema Mnyeti

Huku mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza ahadi ya kujenga barabara ya Sengerema-Nyehunge kwa kiwango cha lami.

Kwa upande mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu licha kushukuru barabara ya Sengerema--Nyehunge kujengwa kwa kiwango cha lami bado ameomba barabara ya Sengerema-Kamanga  sambamba na barabara ya Busisi-Ngoma nazo zijengwe kwa lami ili ziwasaidie wananchi wa maeneo hayo kuinuka kiuchumi.

Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema wananchi wanapaswa kupongeza jihada zinazofanywa na serikali kuboresha miundombinu ya barabara.

"Leo barabara ya Sengerema -nyehunge imetiwa Saini kujengwa kwa lami hii ni hatua Serikali imefanya na itaendelea na mkakati huo,” amesema Kasekenya.

Mmoja wananchi wa wilayani Sengerema Anastazia John amepongeza hatua ya Serikali ya kuamua kufungua uchumi wa  wakazi wa eneo hilo baada ya utiaji saini wa ujenzi wa lami wa barabara hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live