Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makonda kupita nyumba kwa nyumba kupima tezi dume

6842 29739828 476908346073401 5438701547733123072 N TZW

Sat, 21 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema ana mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba ili kuwapima wanaume saratani tezi ya dume.



RC Makonda amebainisha hayo leo Aprili 21, 2018 wakati akifungua warsha ya chanjo hiyo. Amesema tezi dume inaumiza zaidi kina baba lakini hakuna mwamko wa kulizungumzia jambo hilo katika jamii.

“Kuna kasumba kuwa saratani ya tezi dume inapimwa kwa kidole jamani sio kweli, kuna kipimo cha damu na ni rahisi hivyo nina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu kuhakikisha hii kasi ya vifo kwa kina baba inapungua kwa kuwagundua mapema na kuwaanzishia matibabu,” amesema RC Makonda.

RC Makonda amewataka kuzingatia kupata chanjo kamili kwa kurudia mara ya pili ili kuikamilisha na kuepuka ugonjwa huo. Siku ya Jumatatu, April 23, 2018 kuna tarajiwa kuanza kutolewa kwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14.

Chanzo: bongo5.com