Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makonda avalia njuga uhaba wa madarasa

35394 Pic+makonda+2 RC Makonda avalia njuga uhaba wa madarasa

Wed, 9 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanafunzi wa kidato cha kwanza 31, 092 waliokosa nafasi ya vyumba vya madarasa waendelee kufika vituoni kwa ajili ya kujiandikisha.

Amesema wanafunzi hao sawa na asilimia 47, waripoti vituoni mapema wakati ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa 622 ukiendelea kuandaliwa.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumanne Januari 8, Makonda amesema idadi hiyo ya wanafunzi ni wale waliofaulu na kukosa nafasi kutokana na kukosekana kwa vyumba hivyo vya madarasa.

“Serikali itahakikisha wanafunzi wote waliofaulu katika mkoa wa Dar es Salaam wanajiunga na kidato cha kwanza kama ilivyokusudiwa, tunachofanya viongozi ni kuhakikisha tunajenga kwa haraka na kukarabati vyumba 622,” amesema.

Jumla ya watahiniwa 70,303 walifanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2018 na kati yao 64,861 sawa na asilimia 92 walifaulu kujiunga na kidato cha kwanza.



Chanzo: mwananchi.co.tz