Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makonda aanza kumjengea Bi Penina nyumba

Makondazzzz RC Makonda aanza kumjengea Bi Penina nyumba

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda ameanza utekelezaji wa ahadi yake ya kumjengea Bibi Penina Petro (70) nyumba ya vyumba vitatu na sebule huko Siwandete Kata ya Kiranyi wilayani Arusha.

Makonda aliahidi kumjenga nyumba Bibi huyo wakati wa kliniki yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Arusha ambapo Bibi huyo alilia mbele yake na kueleza shia ya nyumba yake kudondoka na Ndugu zake kugoma kumjengea nyumba mpya kutokana na kutojaliwa kupata Mtoto na hivyo kudai kuwa hakuna haja ya kumjengea nyumba mpya kwani hana muda mrefu wa kuendelea kuishi Duniani na hatokuwa na Mrithi.

Tayari Wataalamu wa ujenzi wamefika kwenye eneo la Bibi huyo kwa ajili ya upembuzi wa awali na kupima eneo hilo na kulingana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ujenzi wa nyumba hiyo unatarajiwa kuanza wiki hii.

Bibi Penina ametumia fursa hiyo kumuombea kheri na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali wanyonge na kuwa majibu ya changamoto zao huku pia akimshukuru Mkuu wa Mkoa Paul Christian Makonda kwa kuja na kliniki ya kuwasikiliza na kutatua changamoto za Wananchi pamoja na kuwa na nidhamu katika kuahidi na kutekeleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live