Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla kuhusu wafanyabiashara kujisajili kulipa kodi

Makala Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wametakiwa kusajili biashara zao ili kuhakikisha wanalipa Kodi ambazo zitasaidia kukuza maendeleo nchini.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makalla wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usajili wa walipa kodi wapya jijini Dar es Salaam. Amesema kampeni hiyo inalenga kuongeza ukusanyaji wa mapato kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

Makalla alishauri wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kusajili Bishara zao, jambo ambalo litasaidia kuongeza ukuaji wa uchumi.

" Kupitia kampeni hii, wafanyabiashara tunzeni taarifa za mauzo ili kuisaidia Mamlaka kurahisisha kukadiria kodi na kutoa stakabadhi kwa wateja wenu" alisema Makalla.

Kwa Upande wake Kamishina wa Kodi za Ndani TRA Hurbert Kabyemela alisema kampeni hiyo ni muhimu kwa wafanyabiashara kwani itaongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato yanayotokana na walipa kodi, na inalenga kuwatambua wafanyabiashara wapya wanaojisajili na walipa kodi kote nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live