Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewaelekeza Wakala wa Mabasi ya Mwendokasi DART kuheshimu maamuzi ya kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa iliyotaka wakala hao kutafuta eneo jingine la kujenga Karakana ya mabasi ya Awamu ya tatu kutoka katikati ya mji kuelekea Gongolamboto na kuachia eneo lililokuwa limepangwa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda Cha Vioo kitakachotoa ajira kwa zaidi ya watu 6,000.
Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makalla kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara ya BRT Awamu ya tatu ambapo ameshangazwa kuona Wakala hao wanaendelea Kung'ang'ania eneo Hilo licha ya kushiriki kwenye kikao Cha kamati ya Ulinzi na usalama na kuridhia maelekezo Ya kamati.
RC Makalla amesema kikao Cha kamati kiliona ni busara eneo kutumika kwa ajili ya kiwanda kitakacholeta tija kwenye uwekezaji, Ajira na kuwezesha Serikali kupata mapato tofauti na kulaza magari.
Kutokana na hilo, RC Makalla amewaelekeza DART kushirikiana na Halmashauri ya Jiji hilo kutafuta eneo lingine watakalolipa Wananchi fidia Ili kujenga Karakana hiyo.
Pamoja na hayo Makalla amesema yayari Bank ya Dunia imeridhia kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho na tayari Mwekezaji amefanya Maandalizi ya awali eneo.h