Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amepongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuhamasisha vikundi, Kampuni binafsi na Familia kujiunga na mfuko huo.
Hayo ameyasema mara baada ya kutembelea Banda la NHIF katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashaya yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam. Amewashauri wapeleke huduma hizo kwa watu wenye hali za chini ambazo kwa gharama ambazo zinavumili ili kufikia dhima ya Serikali ya bima ya Afya kwa wote.
Makalla amesema kuwa yeye hajawahi kufika Ofisi za Mfuko huo wa Bima za Afya kwa sababu anatuma maombi kimtandao, hivyo amewaasa watanzania wengine kujiunga kwa kujaza maombi ya kupata bima ya afya kieletroniki na unapewa kadi yako.
Akizungumzia ushiriki wa Mfuko katika Maonesho hayo, Meneja Uhusiano wa NHIF, Anjela Mziray amesema kuwa, Mfuko umejipanga kurahisisha zaidi huduma kupitia mitandao kutoa huduma bora na za haraka kwa wananchi lakini pia kuhamasisha wajiunge na huduma ili wawe na uhakika wa matibabu wakati wote.
"Nawakaribisha wote wanachama na wasio wanachama kutembea banda letu la NHIF ambalo liko karibu kabisa na mlango Mkuu wa kuingilia ndani ya viwanja vya maonesho, NHIF tupo tayari kuwapa huduma ya elimu, kuwasajili na kutatua changamoto wanazokutana nazo katika kupata huduma." Amesema Anjela
Kwa upande wa Wananchi na Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wamefurahishwa na uboreshwaji wa huduma za Mfuko huo ambazo kwa sasa zinapatikana kwa njia ya kielekroniki.
Akizungumzia kuridhishwa kwa huduma hizo, Andrew Elias ambaye alifika katika banda la NHIF kwa lengo la kupata huduma ya elimu na kujiunga na huduma za Mfuko.
"Ukweli huu ni bunifu sana, nimeona ambavyo mmerahisisha mambo ambapo kwa sasa taarifa zote za uanachama zikiwemo gharama unazotumia hospitali, huduma ulizopewa na namna kadi yako iluvyotumika unazipata kupitia NHIF App haya ni mafanikio makubwa." Amesema Elias.
Mkazi wa Kipawa, Roida Msembu ambaye alifika kwa lengo usajili, amesema kuwa gharama zinazotozwa na Mfuko zimezingatia uhalisia wa vipato vya wananchi hivyo akauomba Mfuko kufika katika maeneo mengi zaidi.