Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ametoa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Temeke kupitia kitengo Cha Uhandisi kukamilisha michoro ya Ujenzi wa madarasa ya gorofa Shule ya Msingi Buza ili kukabiliana changamoto ya ufinyu wa eneo.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara Shuleni hapo na kujionea changamoto mbalimbali ikiwemo Uhaba wa Matundu 100 ya Vyoo, upungufu wa Madarasa 62 na Madawati 657.
Upungufu huo umetokana na Shule kuwa na idadi kubwa ya Wanafunzi Kutokana na uamuzi wa Serikali kufuta ada kuanzia Msingi mpaka kidato Cha sita mbapo Shule ya Msingi Buza pekee Ina jumla ya Wanafunzi 4,515.
Aidha RC Makalla ameelekeza Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha Maeneo ya Shule yanapimwa na kuwekewa mipaka/uzio ili kutatua changamoto ya uvamizi wa maeneo ya Shule.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Viwanja vya Michezo yabaki kwa Matumizi hayohayo na sio Ujenzi wa madarasa.