Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla asikitishwa na vitendo vya ukatili

MAKALLA 1 RC Makalla asikitishwa na vitendo vya ukatili

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amos Makalla amesikitishwa na vitendo vya ukatili vinavyosababishwa na imani potofu za wananchi zinazochangia kuongezeka kwa mauaji katika mkoa wa Mwanza.

Amesema imani potofu kwa wananchi zinasababishwa na waganga wa kienyeji kuwadanganya watu kuwa wanauwezo wa kuwapa utajiri na kuwarudisha wapenzi wao jambo ambalo amedai ni la uongo linalopaswa kukemewa.

"Unaenda kwa mganga anakujaza mambo mengi angalia hali yake, ana gari, ana nyumba ya aina gani hali yake ikoje kwanini yeye asingekuwa tajiri, mfano mganga anakuambia mimi nakupa dawa ya kumrudisha mpenzi wako aliyekukimbia alafu yeye mwenyewe amekimbiwa na mke wake kama hiyo dawa inafanya kazi kwanini asijiwekee mwenyewe," amesema Makalla.

Mkuu wa mkoa ameeleza hayo wakati jeshi la Polisi nchini lilipokuwa likitoa mafunzo ya pamoja kati ya jeshi la hilo, watendaji wa kata, viongozi wa dini , madiwani na wenyeviti wa mtaa yenye lengo la kuwajengea uwezo jinsi ya kushirikiana katika kubaini, kuzuia na kukabiliana na uharifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live