Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla amaliza mgogoro wa barabara Kigamboni

WhatsApp Image 2022 12 16 At 19.jpeg RC Makalla amaliza mgogoro wa barabara Kigamboni

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameagiza barabara iliyokuwa ikileta mgogoro eneo la Kimbiji katika Manispaa ya Kigamboni baada mwekezaji kampuni ya ASM kujenga ukuta na kuifunga ifunguliwe.

Ametoa maagizo hayo leo Desemba 16,2022 alipofanya ziara ya pili kwenye eneo hilo la mgogoro na kufanya kikao cha pamoja kati ya wawekezaji wa maeneo hayo, wananchi, viongozi na wataalam wa ardhi kutoka Manispaa ya Kigamboni pamoja na Wizara ya Ardhi.

" Baada ya kupitia vielelezo vya ramani ya mipango miji toleo la mwaka 2021, tumeona hakuna uhalisia wa kuanzisha barabara mpya, tumeona barabara ni hii ya zamani inafaa, sasa nimeagiza leo hii huyu mwekezaji aandikiwe barua na imfikie leo hii kumtaarifu juu ya uwamuzi huu," amesema Makalla.

Ameongeza kwa kuwa tathimini ya awali ya kumlipa fidia mwekezaji huyo ilishafanyika, mchakato huo uendele na ASM alipwe fidia ili barabara hiyo ianze kutumika."Gharama ya kuanzisha barabara mpya ambayo tumeonyeshwa hapa ni kubwa zaidi kuliko kumlipa fidia huyu mwekezaji, sasa maamuzi ya kikao tulichofanya ni hayo, utekelezaji wa kulipa fidia uanze mara moja, tumefanya hivi kwa manufaa mapana ya nchi."

Mgogoro huo wa ardhi umedumu kwa zaidia ya miaka saba ambapo umetokana na mwekezaji kampuni ya ASM (T) Ltd anayemiliki viwanja pacha vinavyotazamana kijiji cha Mikenge kata Kimbiji kuziba barabara inayoelekea kwenye fukwe ya bahari na kwa wawekezaji wengine.

Wananchi na wawekezaji wengine ambao walikosa barabara ya kupita walilalamika kwa Manispaa ya Kigamboni na kuomba barabara hiyo ifunguliwe.

Hata hivyo uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kwa kushirikiana na mwekezaji ASM walianzisha barabara nyingine iliyopita kando ya mto unaomwaga maji baharini kitendo ambacho wananchi na wawekezaji wengine walikipinga.

Akizungumza baada ya maamuzi hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mikenge, Lameck Mayala, amesema uwamuzi huo ni wa busara na waliusubiri kwa muda mrefu.

"Kiukweli tunaishukuru sana Serikali kupitia kwa mkuu wetu wa Mkoa kwa maamuzi haya, hii barabara ilikuwepo kwa miaka mingi sana, ni barabara ambayo inawawezesha wananchi kufika baharini ambako wanafanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato,pia wapo wawekezaji walitoa ajira kwa vijana wetu kwenye hoteli zao walishindwa kufika kwenye maeneo yao, tunashukuru kwa maamuzi haya ya Serikali," amesema Mayala.

Aidha, mmoja wa wawekezaji anayemiliki hoteli maeneo hayo ambaye biashara yake iliathirika kutokana na kufungwa barabara hiyo, Vidate Msoka, alisema maamuzi hayo yatawafanya kuendelea na biashara zao na kuchangia pato la taifa kwa kulipa Kodi.

"Biashara zetu zilisimama kwa muda, hatukuwa tunapata wateja kwa sababu ya kukosekana barabara ya kutufikisha hotelini, maamuzi haya yametupa faraja kubwa, tunashukuru" amessema Vidate.

Hata hivyo kwenye kikao hicho kilichokuwa chini ya Mkuu wa Mkoa Makalla, mwekezaji ASM hakuhudhuria licha ya kupewa taarifa na badala yake alitumia mwakilishi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live