Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla aipongeza Ubungo Madarasa ya Samia

WhatsApp Image 2022 12 14 At 12.jpeg RC Makalla aipongeza Ubungo Madarasa ya Samia

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kufanya vizuri katika ujenzi wa Madarasa ya Mama Samia Suluhu Hassan.

RC Makalla amezungumza hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa Madarasa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo Leo alikuwa katika Wilaya Ubungo.

RC Makalla amesema Ubungo wamefanikiwa kujenga majengo 27 yaliyo kamilika Kati ya 80 ambayo walikuwa wamepangiwa.

"Wote walipewa pesa kwa pamoja lakini Ubungo wamekuwa wa kwanza kumaliza kuzidi wenzao maana hao wengine Kama wanasema wao Madarasa Yao ni mengi wangemaliza angalau haya 27 kama Ubungo" Amesema RC Makalla.

Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imepokea kiasi Cha Shilingi Bilioni 1.62.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live