Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla afunguka "uvaaji wa barakoa kwenye vyombo vya usafiri ni lazima"

WhatsApp Image 2021 07 26 At 12.46.46 PM 660x400.jpeg RC Makalla afunguka "uvaaji wa barakoa kwenye vyombo vya usafiri ni lazima"

Mon, 26 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona ambapo amepiga marufuku Wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.

.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya ambapo amesema watafanya ziara za kustukiza kwenye Vituo vya Daladala, Feri, Stendi, Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya Masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia Utekelezaji wa agizo hilo.



Aidha RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutoa huduma Bora za matibabu kwa wagonjwa wote watakaofika hospital na kuwataka Wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya Afya.
Chanzo: millardayo.com